Sunday, January 14, 2018

MKURUGENZI MTENDAJI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH), APOKELEWA KWA NDEREMO SHEREHE YA KURUGENZI YA UUGUZI NA UKUNGA

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa. Lawrence Museru alianza kwa Kumshukuru Mungu sana sana sana na kusema, nduguzangu nawashukuru sana,ila nitakuwa sina mengi ya kusema ila napenda kutoa shukrani zangu kwa waandaaji wa sherehe hii kwa kunikaribisha kuwa nanyie hapa, aliendelea kusema.
 Nimefarijika kuwa kukutana hapa tukiwa nje ya kazi zetu kwa pamoja tukiwa wazima na mkaona mnikaribishe ili nijumuike nanyie nasema asanteni sana ila leo si siku ya kuongea leo ni siku ya kufurahi ila sababu mmenikaribisha nikiwa kama kiongozi wenu naomba niseme mawili matatu.
 Niseme kwamba Tunatambua nafasi ya Wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, sisi kama viongozi wenu  tunatambua umuhimu wa Wauguzi pale tunapotoa huduma pia tunatambua changamoto ninyingi katika utoaji huduma wenu na kwamba kunamambo mengi sana mngependa yafanyiwe kazi ili  kusudi muweze kutoa huduma inavyotakiwa na kwanamna moja au nyinyingine hatujaweza kutatua.
 Lakini mmeendelea kutoa huduma kwa nguvu kabisa na ufasaha mkubwa sana alisema Museru.Tunaposikia Muhimbili sasa wanatoa huduma nzuri na ambayo watu wanaridhiakanayo ni kwasababu ya Wauguzi wanatekeleza wajibu wao na ningependa kuwaomba na kuwasihi kuendelea kutoa huduma kama ambavyo kiapo chenu kinavyo elekeza na wengiwetu tunatoa huduma kama inavyotakiwa kutolewa, alisema Museru
 Ndio maana sisi kama viongozi kwa kiasi kikubwa sana tunajitajitahidi kutatua matatizo yanayo wakabili ninyi katika utoaji huduma kama matatizo ya vitendea kazi, matatizo ya mazingira yenu mnayotolea huduma pia na matatizo ya stahiki zenu, na mimi pamoja na Mkurugenzi wa Uuguzi pamoja na viongozi wengine tumekuwa tukipigania na kuhakikisha Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili anapata stahiki inayostahili katika utoaji huduma.
Kuna ambayo tumefanikiwa na mengine hatujafanikiwa ila tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu na kuhakikisha Muhudumu na Muuguzi wa Hospitali ya taifa Muhimbili anapata stahiki yake anayostaili, sasa mimi niwaombe sisi sote.
  Paletunapotoa huduma tuhakikishe tunatoa huduma kama inavyo takiwa na tuhakikishe tunatatua kero za wateja wetu ambao ni wagojwa na kuhakikisha wanahudumiwa ipasavyo na kutoa  wito kwa wale wachache kwani  kwenye mazuri hapawezi kukosa doa alisema mseru.
Tujaribu kuwarekebisha sisi tunao fanyanao kazi na viongozi tunao wasimamia ilikusudi wale wachache wanao chafua jina la Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wazidi kupungua na mwishowe wote waishe na tutoe huduma inayokubalika.

Nimefurahi sana kuwaona ndugu zetu wa Kyuba, naona sasa wanaongea kiswahili kwani nilikuwa na bahati ya kwenda kule kwao wakati tulipokuwa tukitafuta watu wakuja fanyanao kazi na kama mnavyo waona ndivyo walivyo na wengine tunafanana nao na kunawengine ni tofauti na sisi kwa rangi 
Ila niseme hawa ndugu zetu tutakaanao kwa miaka miwili au tunaweza kukaanao zaidi na ninawaomba muwakubali sehemu ambazo tunazofanyanao kazi, tujifunze hasa jinsi wanavyotoa huduma na wao kama kunachakujifunza tuwafundishe alisema
  Museru.
Nduguzangu ninafuraha kwa
kuuaga mwaka wa 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, tukiwa wote na tunapo ingia mwaka huu niwapongeze kwa kuiweka Hospitali ya Taifa katika ramani. Hospitali ya Taifa Muhimbili ni Hospitali kongwe hapa nchini kama jina linavyo jieleza na tuhakikishe malengo hayo tunayafikia 

Mwakajana tulifanikisha kutoa huduma ambazo zilikuwa zikitolewa nje ya nchi na sasa zinafanya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tunapo ingia mwaka huu wa 2018 niwaombe kama mlivyosema
katika risala naomba tuzidi kuipaisha na kuiweka katika ramani ya ulimwengu Hospitali ya Tafa Muhimbili na nipende kuwashukuru kwa ushirikiano wenu na asanteni sana.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Wauguzi wakifurahia baada ya kuwashinda wanaume katika mchezo wa kuvuta kamba
Wauguzi wakicheza karata ufukweni mwa Bahari ya Hindi Ununio

Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili akiruka kamba ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Ununio
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakicheza mpira


Mmoja wa mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiogelea ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Ununio Dar es Salaam
Afisa Muuguzi Hospiatali ya Taifa, Halima Mayumana akiudaka mpira wakati wa Sherehe ya  kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga ya kuuaga mwaka 2017 na kuupokea mwaka wa 2018 iliyofanyika Ukumbi wa Ukumbi wa Pink Diamond Bahari Beach Dar es Salaam.







Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akicheza mchezo wa kuruka kamba ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Ununio Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi  ya kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga, Segla Mgaya akiwashukuru Wauguzi kwa kujitoa kwa hali na mali kuwezesha kufanikisha Sherehe hii, napenda kuwashukuru wote waliojitoa na kuwashukuru wafadhili wetu, Mobisol na Anchor desing, Sherehe iliyofanyika katika  Ukumbi wa Pink Diamond Bahari Beach .

Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Petro Jilatu akiwapongeza Wauguzi zaidi ya mia mbili  katika kufanikisha Sherehe hiyo sambamba na Sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar kwani Sherehe yetu ni kucheza michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba, kuogelea na kucheza karata, yote hayo nikatika kuhakikisha tunabadilishana mawazo kwani katika sherehe hii kutakuwa na wakurugenzi zaidi ya watano akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Profesa. Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Uuguzi Bi, Agnes Mtawa. Sherehe iliyofanyika 12 Januari 2018, katika Ukumbi wa Pink Diamond Beach Dar es Salaam
Baadhi ya Wauguzi katika pozi ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Ununio


Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea






































Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga Bi Angnes Mtawa alianza kwa kumshukuru Mungu na kuwashukuru wote walioshiriki katika kujitoa kwa kufanikisha sherehe japo vipato vyetu si vidogo
lakini mmeweza kufanikisha sherehe hii na tumejitoa na pale mlipotoa Mungu akapajaze mara miamoja.Mkurugenzi Mtawa alisema, nawashukuru kwa ushirikiano kwa sababu tupo hapa kada
mbalimbali na leo hatuzungumzi huyu nani wala huyu nani bali tunazungumza wote tupochini ya Kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga kwahiyo nawashukuruni sana na ninawapongezeni sana na baada
ya kuyasema hayo nawaombeeni baraka teleteletele kwa Mungu, tuendelee kutenda mema na kutoa huduma kwa bidii na kubarikiwa katika mwaka 2018, uwe mwaka wa mafanikio asanteni kwa kunisikiliza.

Wauguzi wakibadilishana mawazo
Wauguzi (katikati) wakisalimiana wengine wakishuhudia

Wauguzi wakichangamsha viungo kwa kucheza
Wauguzi kwa umoja wao wakimuingiza Ukumbini Mwenyekiti wakamati ya Sherehe hiyo, Segla Mgaya (wa nne kulia)








Mkuu wa Idara Uuguzi na Mazingira wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa vitengo mbali mbali katika Hospitali hiyo
Afisa Muuguzi, Kalunde Shabani akiwapatia wauguzi wenzake keki baada ya kuikata katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na Sherehe ya wauguzi iliyofanyika  Ukumbi wa Pink Diamond Bahari Beach .













Kipekee tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa juhudi zako kubwa unazozifanya kuipaisha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuiweka katika ramani ya ulimwengu, Sisi tunakuahidi kukupa ushirikiano wetu wa hali na mali ili kuhakikisha malengo ya Hospitali yetu yanafikiwa, Hayo yalisemwa na Muuguzi wa Hospitali hiyo wakati akisoma risala, Kalunde Shabani,ambapo aliendelea kusema,Ndugu mgeni rasmi mbele yako kunawafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kada mbalimbali ikiwemo kada ya Uuguzi, Wahudumu wa afya wasaidizi, Ustawi wa jamii, Nutrition ambapo hawa ni wawakilishi, kwani inabidi huduma ziendeleekutolewa.Ndugu mgeni rasmi tumeungana kwa pamoja ilikufanikisha sherehe hii tukiwa na madhumuni ya kuchangamsha akili kwa kubadilishana mawazo na kubadilisha mazingira kutokana kazi kubwa iliyopo mbele yetu ya kutoa huduma kwa wagonjwa na jamii yetu.ndugu mgeni rasmii iliundwa kamati iliyojumuisha wajumbe kutoka kila jengo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kamati hii ilianza vikao vya mandalizi mara moja.vikao vilianza rasmi chini ya uongozi wa Mwenyekiti, Segla Mgaya,ambapo wajumbe wote walifanya mandalizi ya sherehe hii kwa weledi waao kwa kujitolea kwa hali na mali.Ndugu mgeni rasmi sherehe hii imewezeshwa na wafanyakazi pomoja na baadhi ya wafadhili ambao ni Mobisol na Anchor desing katika kufanikisha sherehe hii.Ndugu mgeni ramii pamoja na mafanikio ya sherehe kulikuwa na changamoto chache wakati wa maandalizi kama vile; mawasiliano hafifu baina yetu
na kutoa mapendekezo wa uhamasishaji wa taarifa na ifahamike sherehe hii ni ya wafanyakazi wote waliopo chini ya kurugenzi Uuguzi na Ukunga na mwisho nikushukuru wewe kwa kukubali mwaliko wetu na tumefarijika sana kuwa nasi katika sherehe hii
na kuwashukuru wageni waalikwa na wadau mbalimbali.





















Afisa Muuguzi, Kalunde Shabani (katikati) akimlisha kipande cha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Lawrence Museru katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na Sherehe ya wauguzi iliyofanyika  Ukumbi wa Pink Diamond Bahari Beach


Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru (wa tatu kulia waliokaa) akipata picha ya pamoja na viongozi wa vitengo mbalimbali wa Hospitali hiyo

Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru (wa pili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi na wauguzi wa Hospitali hiyo

Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru (wa pili kushoto walio kaa) na Wakuu wa Vitengo mbalimbali wa Hospitali hiyo wakipata picha ya pamoja

Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru (katikati) akipata picha ya pamoja na Wauguzi na wakuu wa vitengo mbalimbali wa Hospitali hiyo

Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru (wa pili kushoto), katika  picha ya pamoja na Wauguzi wa Hospitali hiyo ambao wanatoka Kyuba


 Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wilson Lomnyaki (wakwanza kushoto) akimkabidhi Zawadi  Mkurugezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili profesa, Lawrence Museru iliyoandaliwa na kamati ya Sherehe hiyo na kulia ni Mhasibu wa Kamati ya Sherehe hiyo, Matilda Mrina  akimkabidhi zawadi,  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga Bi Angnes Mtawa  



Mkuu wa Jengo la Magonjwa ya nje, Juni Samweli (kulia)   akifurahia jambo  wakati  wa Sherehe hiyo