Aliyekuwa
Kiongozi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Josephine Lwambuka amewaomba
wafanyakazi hao hasa walio katika kitengo hicho kwa kujituma na kujitoa
kwa kufanya kazi na kusimamia misingi ya sheria na kanuni kwa kufanya
kazi kwa bidii.Lwambuka aliyasema hayo wakati alipokuwa akipongezwa kwa
kuagwa na wafanyakazi wa kitengo hicho alichokuwa akikitumikia kama
kiongozi alisema , Nduguzangu ninawaomba mshirikiane kwa umoja katika
majukumu ya kazini na muwe wamoja na kupendana bila kubaguana na msiweke
makundi yoyote, pia alisema, Lwambuka. Naomba niwaambie kwa mtu yoyote hakuna anaye muona ila Mungu anamuona kwa kila hatua, hivyo mfanyapo kazi msimsahau Mungu na kutosahau Ibada nawaomba hasa vijana kufanya kazi kweli na akatoa tano akisema, Mimi mwenyewe toka nianze kufanya kazi na hadi Nastaafu sijawahichukua kitu chochote kwa mgonjwa au kwa ndugu wa mgonjwa (Rushwa) na pia nawaombeni kusema ukweli daima kwani ukiwa muongo utakuja sahau ulicho kisema hatimae unaingia katika jambo ambalo lilikuwa lahitaji ukweli pasina kuficha, nawaomba muwe wakweli na uongo muutenge mbali katika kufanya kazi kwa kumsaidia Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali yetu ya Taifa,Nawaombeni mshirikiane kwa umoja na mumtangulize Mungu mbele mtafanikiwa bila kusahau kujishughulisha na kitu mbadala si kutegemea mwisho wa mwezi asanteni sana kwa kunifanyia shughuli namuomba Mungu awazidishie, pale mlipopunguza azidishe bila idadi nawapenda wote asanteni. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) | |||||||||||||
Mstaafu,
Josephine Lwambuka akiwa katika picha ya pamoja katikati na aliye
achiwa kijiti cha Kitengo cha magonjwa ya dharula chumba cha Upasuaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Faustina Kissinde kushoto na Kiongozi
Msaidizi wa Kitengo hicho Mama Mchungaji, Flora Ndulango kulia
Mstaafu,
Josephine Lwambuka katikati akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake
na baadhi ya marafiki na wafanyakazi wa Hospitali ya taifa Muhimbili
(MNH)
Mstaafu, Josephine Lwambuka akiingia ukumbini
Rafiki kipenzi wa Mama Lwambuka, Joyce Chirwa akipungia mikono waalikwa mara alipotambulisha
Mstaafu,
Josephine Lwambuka (wa pili kushoto) akijiburudisha na wafanyakazi wa
Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), wakati alipokuwa akipongezwa katika ukumbi wa Salender
Pub uliopo Upanga, Hafla iliyo andaliwa na Wafanyakazi wa Kitengo hicho
Mstaafu, Josephine Lwambuka (wa pili kulia) akicheza na wafanyakazi hao
Kiongozi
Msaidizi Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Mama Mchungaji, Flora Ndulango (kulia)
akifungua sherehe kwa Sala
Muuguzi
katika Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Charles Maungu akitambulisha baadhi ya
wafanyakazi hao waliofika katika hafla hiyo
Mstaafu, Josephine Lwambuka (katikati) akipungia mikono wageni waalikwa mara baada ya kutambulishwa na Muuguzi katika Kitengo
cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Charles Maungu (pichani hayupo).
Mkuu
wa Kitengo cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Faustina Kissinde akipungia mikono wage waalikwa katika hafla
fupi iliyoandaliwa na kitengo hicho ambapo katika kamati hiyo alikuwa
Mwenyekiti
Mkuu
wa Kitengo cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Faustina Kissinde alianza kwa kumshukuru Mungu kufikia hapo
walipofikia yeye na kamati yake yote na kusema namuomba Mungu azidishe
umoja na upendo kati yetu na pili namshukuru muagwa mama, Lwambuka kwa
malezi na ushauri wake na nitahakikisha hakuna hata mmoja nitakaye
mpoteza kati ya watu ulio niachia kwani nitahakikisha anashirikiana nao
kwa hali na mali, Kisinde alisema, Jambo la kujivunia kwa mama huyu ni
kuiga yale yote mazuri aliyokuwa akiniambia kabla ya kustaafu kwake,
kwanza kujitoa, kujitambua kama ni kiongozi niwazi kusikiliza ushauri na
mawazo mazuri na kutatua changamoto na kuwasikiliza wafanyakazi
wenzangu, Mama Lwambuka nitakuomba usisite mara nitapokuja kwako kuomba
ushauri alisema kissinde.
Mstaafu,
Josephine Lwambuka (katikati), akigonganisha Glas na baadhi ya
wafanakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharula chumba cha Upasuaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa hafla fupi ya kumpongeza kwa
kustaafu kwa mujibu wa sheria katika Ukumbi wa Salender Pub uliopo
Upanga
Mmoja wa wafanyakazi katika kitengo hicho akicheza mziki wa kwao wa kiasili akirukaruka mfano wa chura
Mstaafu, Josephine Lwambuka (katikati), akigonganisha Glas na baadhi ya wafanakazi wa Kitengo cha
magonjwa ya dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili
wakati wa hafla fupi ya kumpongeza kwa kustaafu kwa mujibu wa sheria
katika Ukumbi wa Salender Pub uliopo Upanga
Mkuu wa Kitengo
cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Faustina Kissinde (kulia) akishirikiana kukata Keki na aliye wahi kuwa Mkuu wa kitengo hicho, Josephine Lwambuka
Aliyekuwa Kiongozi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Josephine Lwambuka akilishana kipande cha Keki na
Kiongozi Msaidizi Kitengo Mama Mchungaji, Flora Ndulango kwa mtindo wa kuukaribisha mwaka 2018
Kiongozi
Msaidizi Kitengo cha Magonjwa ya Dharula Chumba cha Upasuaji Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Mama Mchungaji, Flora Ndulango (wapili
kushoto) akiongozana na wafanya kazi wenzake kumpongeza aliyekuwa Mkuu
wa Kitengo hicho, Josephine Lwambuka
Baada ya kutunzwa Mstaafu, Josephine Lwambuka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi hao
Mkuu
wa Kitengo cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Faustina Kissinde akiongoza
wafanyakazi wenzake kwenda kutoa zawadi ya kitengo chake iliyoandaliwa
na kamati
Mkuu wa Kitengo
cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Faustina Kissinde akiongoza wafanyakazi
wenzake kwenda kutoa zawadi ya kitengo chake iliyoandaliwa na kamati, Mstaafu akikabidhiwa bahasha kwa mstaafu, Josephine Lwambuka (kushoto)
Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo
cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Josephine Lwambuka akibebwa juu kwa ishara ya kuonyesha kumkubali katika utendaji wake wa kazi
Rafiki Kipenzi wa Mstaafu Mama Lwambuka akizungumza jambo katika hafla hiyo
Mkuu wa Kitengo
cha magonjwa dharula chumba cha Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Faustina Kissinde akiwashukuru wote walio husika na kufanikisha Sherehe hiyo
No comments:
Post a Comment